PATA MAARIFA ZAIDI JUU YA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI NA TIBA YAKE

 Dysmenorrhea ni nini?
  
Dysmenorrhea ni maumivu wakati wa hedhi, kuna maumivu ya aina mbili;

  • Primary ambayo ni maumivu ya kawaida  na secondary ambayo ni maumivu yanayotokea baada ya kupata maradhi au ugonjwa sehemu ya mfumo wa uzazi(reproductive organs)


PRIMARY Dysmenorrhea
  • haya ni maumivu ya kawaida na huanza siku ya 1 au 2 kabla au baada ya damu kuanza kutoka 

(bleeding ), na huisi maumivu sehemu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu kwa ilivyozoeleka,

  • maumivu  ya mgongo hasa maeneo ya kiuno au sehemu za mapaja

  • Maumivu yanawezo yakaanza kutoka yakawaida mpaka makali na yanaweza isha kati ya masaa 12 hadi 72 yaani siku moja hadi tatu na yanaweza kuambatana na kichefuchefu,na kutapika , uchovu na wakati mwingine kuharisha

  • Mara nyinyi au kawida primary dysmenorrhea huwa na maumivu kidogo  na wakati mwingine kupotea kabisa /kusimama pindi mwanamke apatapo mtoto


SECONDARY Dysmenorrhea
Hii hutokea baada ya sehemu za mfumo wa uzazi kupata maradhi au ugonjwa kama ifuatayo;

  • Endometriosis huu ni ugonjwa ambao tissues ambazo zinapatikana kwenye mji wa uzazi(uterus) zinakuwa zinapatikana inje ya mji wa uzazi

  • Adenomyosis hili ni tatizo ambalo hutokana na sehemu zinazofunika(lining) sehemu za ndani ya mji wa uzazi kukua(grows) kwenye misuli(muscle) ya mji wa uzazi

  • PID( pelvic inflammatory disease) ni ugonjwa unaotokana na uvimbe wenye maumivu au kuvimba kwenye Fupanyonga na hii husababishwa na backeria

  • Cervical stenosis hii ni hali ambayo sehemu ya mlango wa uzazi kuwa nyembamba kuliko ilivyokawaida

  • Fibroid(benign tumor)  uvimbe sehemu ya ukuta wa ndani wa mji wa uzazi

NOTE: ukiona maumivu ni makali sana na yanachukua muda kupoa na pia kutoka kwa damu kunakuwa kusiko kwa kawaida  unapaswa kuwa makini sana maana yaweza hayo magonjwa ndo tatizo

DALILI ZAKE

  • Maumivu huanza mapema na huchukua muda mrefu kuisha kuliko yale maumivu ya Primary dysmenorrhea
  • Pia maumivu huwa hayaambatani na kichefuchefu,kutapika,uchovu au kuharisha

TIBA
Primary dysmenorrhea
  •  Ibuprofen 200mg -600mg TDS
             au
  • Acetylsalycilic acid 300-600mg 4hrs

              au
  • Diclofenac 50-100mg TDS or BD

              au

  • Mefenamic acid 500mg TDS

  •   pamoja na Hyoscine butylbromide 20mg 8hrs for 5 days

Hivyo kati ya hizo dawa moja wapo ni lazima utumie pamoja na Hyoscine butylbromide

TIBA SHAURI

  • Weka kitu chenye joto nyororo au kitambaa laini au chupa yenye maji moto sehemu ya chini ya tumbo inayouma na ikipendeza zaidi masseji hiyo sehemu

  • Epuka kula vyakula vilivyo na Caffeine

  • Epuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe

  • Masseji sehemu ya chini ya mgongo na tumbo

  • kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kwani husaidia kupunguza maumivu wakati wa hedhi

NB kwa secondar dysmenorrhea unatakiwa kutibu maradhi au ugonjwa unaosababisha maumivu kuwa sio ya kawaida hivyo kupata historia ya maumivu wakati wa hedhi ni muhimu sana kwani ndo itakuongoza kupata tiba sahihi

                 asante na maoni yanakaribishwa

Comments

Popular posts from this blog

FIRST CAT ONE

monday 2023 evening

cat 1 essay