PATA MAARIFA ZAIDI JUU YA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI NA TIBA YAKE
Dysmenorrhea ni nini? Dysmenorrhea ni maumivu wakati wa hedhi, kuna maumivu ya aina mbili; Primary ambayo ni maumivu ya kawaida na secondary ambayo ni maumivu yanayotokea baada ya kupata maradhi au ugonjwa sehemu ya mfumo wa uzazi(reproductive organs) PRIMARY Dysmenorrhea haya ni maumivu ya kawaida na huanza siku ya 1 au 2 kabla au baada ya damu kuanza kutoka (bleeding ), na huisi maumivu sehemu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu kwa ilivyozoeleka, maumivu ya mgongo hasa maeneo ya kiuno au sehemu za mapaja Maumivu yanawezo yakaanza kutoka yakawaida mpaka makali na yanaweza isha kati ya masaa 12 hadi 72 yaani siku moja hadi tatu na yanaweza kuambatana na kichefuchefu,na kutapika , uchovu na wakati mwingine kuharisha Mara nyinyi au kawida primary dysmenorrhea huwa na maumivu kidogo na wakati mwingine kupotea kabisa /kusimama pindi mwanamke apatapo mtoto SECONDARY Dysmenorrhea Hii hutokea baada ya sehemu za mfumo wa...